Geay alitumia saa 2:06:04 kumaliza mbio zake huku aliyeshika nafasi ya kwanza Evans Chebet kutoka Kenya akitumia saa 2:05:54.

Kupitia ukurasa rasmi wa rais ameandika kuwa “Nakupongeza Gabriel Gerald Geay kwa kuwa mshindi wa pili katika Mashindano ya riadha ya Kimataifa ya Boston yaliyofanyika leo (jana) nchini Marekani. Jitihada zako zimeijengea heshima Tanzania. Nakutakia kheri katika kusonga mbele Zaidi, Serikali itaendelea kuwaunga mkono wanamichezo” ameandika Rais Samia
Leave a Reply