Rais Samia: Nilipowateua Nikki Na Mwana Fa Watu Hawakunielewa

Rais Samia: Nilipowateua Nikki Na Mwana Fa Watu Hawakunielewa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa uteuzi wa wasanii Hamis Mwinjuma (Mwana FA) na Nickson Simon (Nikki wa Pili) katika nafasi za uongozi umekuwa na manufaa makubwa kwa Serikali yake, licha ya mashaka ya awali kutoka kwa baadhi ya watu.

Akizungumza leo, Februari 27, 2025, katika ziara yake mkoani Tanga, ndani ya Jimbo la Muheza ambalo Mwana FA ni mbunge, Rais Samia amesema "Nilipomteua yeye (Mwana FA) na Mkuu wangu wa Wilaya ya Kibaha, Nikki wa Pili, watu hawakuelewa.

Wakasema, 'Mama anateua wachepe hawa, inakwenda kuwaje, hawa wamezoea majukwaa na kurap, watafanya kazi gani? Lakini nataka niwaambie kwamba hawa wananisaidia sana,".

Aidha, amesisitiza kuwa uwepo wa MwanaFA katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo umesaidia sana kufikisha ujumbe kwa vijana kwa lugha wanayoielewa, hivyo kuwaomba wananchi waendelee kumtunza kwa manufaa ya sasa na siku za usoni.

Mbali na wawili hao kuzitumikia vizuri nafasi zao waliwahi kutamba na ngoma kama Safari, Hesabu, Nje ya Box, Gwiji, Mfalme, Bila kukunja goti na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags