Rayvanny aujaza uwanja wa Albania, Ulaya

Rayvanny aujaza uwanja wa Albania, Ulaya

Usiku wa kuamkia leo Juni 28, mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Rayvanny alifanya show katika uwanja wa mpira wa ‘Air Albania Stadium’ na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki wakati alipokuwa akipanda jukwaani. 

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Rayvanny ame-share video akionesha jinsi alivyopokelewa kwa shangwe na mashabiki kwa kumuwashia tochi huku akiweka wazi kuwa uwanja huo ulikuwa ‘sold out’ ambapo unakadiriwa kuingiza zaidi ya watu 20,000.

 Rayvanny alitangaza kufanya show Albania mapema wiki ambapo alitaka kuwafunga midomo wadau wote waliyokuwa wakidai kuwa wasanii wa Bongo wakienda kutumbuiza nchi za watu huwa wanafanya show sebuleni. 

Hata hivyo kupitia instastory ya Chui amedai kuwa ilikuwa ni ndoto yake kutumbuiza mbele ya maelfu ya watu. “Ndoto hutimia asante Mungu ilikua ndoto yangu kuimba kwenye maelfu ya watu na inatimia sold out Stadium in Albania”.

Hii sio mara ya kwanza kwa Chui kupokelewa vizuri na mashabiki utakumbuka kuwa mwaka 2022 alipokelewa kwa shangwe jijini Paris wakati alipokuwa akitumbuiza na msanii kutoka Columbia, Maluma.V






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags