Rich Mitindo Arudi Nyumbani Kwa Watoto Wake

Rich Mitindo Arudi Nyumbani Kwa Watoto Wake

Baada ya Jackline Wolper kutoa taarifa za kuachana na Mume wake kupitia mitandao ya kijamii, Rich Mitindo ameshea videos na picha zikimuonesha amerejea nchini Tanzania akitokea nchini China ambapo amekuwa akiishi huko na kufanya biashara kwa muda mrefu.

Rich ameshea picha akiwa na watoto wake wawili kwenye nyumba yake na Wolper huku akishusha ujumbe usemao…

"Kipimo cha mwanaume sio suruali wala pesa ingawa vyote vinahitajika, kipimo cha mwanaume Hodari ni utu na upendo kwa familia yake haswa watoto wake niliwamis kiukweli" ameandika Mitindo.

Utakumbuka kuwa siku mbili zilizopita Wolper ilitangaza kuachana na mume wake Rich Mitindo ambapo aliweka wazi kupitia ukurasa wake wa instagram akieleza kuwa yupo kwenye mchakato wa talaka japo mpaka sasa Rich hajathibitisha kuachana kwao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags