Mwanamuziki kutoka Marekani Rihanna amefunguka kuwa ameumaliza mwaka 2024 bila ya kuonja pombe ya aina yoyote ile.
Riri ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa instagram kwa ku-share video iliyokuwa ikimuonesha akihesabu dakika zilizosalia kufikia mwaka 2025 huku akijipongeza kwa kutokunywa wala kuonja pombe mwaka mzima wa 2024.
Hata hivyo post hiyo ambayo imepata maoni kutoka kwa mashabiki zaidi ya 5600 ndani ya lisaa wakionesha kuhitaji kazi mpya kutoka kwa msanii huyo ambae anatajwa kuongoza kwa wasanii wakike waliouza zaidi rekodi zao kwa karne ya 21 huku akishika namba 3 kwa wasanii matajiri zaidi duniani 2024.
Rihanna ambae amekuwa kimya kwenye gemu ya muziki kwa muda usiopungua miaka 2 kutokana na kuwa bize na uzazi na malezi ya watoto wake ambao ni RZA & Riot pamoja na biashara zake za Fenty Beaty.
Leave a Reply