Mwandishi wa filamu kutoka Marekani Robert Eggers, ameimwagia sifa filamu ambayo inatizamwa zaidi katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kuitaja kuwa filamu bora ya muda wote kwa upande wake.
Eggers ambaye alitambulika zaidi kupitia uandishi wake kwenye filamu kama The Witch na Nosferatu hivi karibuni alifunguka kuwa filamu hiyo ni bora zaidi kuwahi kutokea.
“Naangalia hii mara moja kwa mwaka Pia nadhani kuwa hii ni shuhuda ya ubora. Ni filamu isiyo na muda. Imewekwa picha kwa ukamilifu. Tofauti na filamu nyingi za aina hii, haijapigwa picha kupita kiasi. Ni filamu iliyojengwa vizuri sana,” amesema Eggers
Home Alone ni filamu iliyotoka Novemba 16, 1990 ikiwa imetayarishwa na Chris Columbus huku lengo la kutengenezwa kwake likiwa ni kuhamasisha watu kuondokana na msongo wa mawazo katika kipindi cha likizo na sikukuu za mwisho wa mwaka.
Ikumbukwe kuwa Columbus na Eggers ni marafiki wa muda mrefu ambapo Columbus alikuwa mshauri mkubwa wa Eggers kupitia filamu yake ya The Witch huku akichukua jukumu muhimu la ubunifu kama mtayarishaji wa Nosferatu.
Leave a Reply