Ronaldo kupunguziwa majukumu Euro 2024

Ronaldo kupunguziwa majukumu Euro 2024

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Wes Brown amesema staa wa Al Nassr na Ureno ajiandae kwa majukumu tofauti na yale aliyozoea katika kikosi cha ‘timu’ ya taifa kwenye mashindano ya Euro mwaka huu.

Ronaldo ambaye atakuwa nahodha wa Ureno kwenye kulisaka taji lao la kwanza la Euro tangu mwaka 2016, anaonekana atapunguziwa majukumu kutokana na umri wake.

Akizungumza na Thrash podcast, Wes Brown alisema: “Nafikiri atakuwa anaanza kikosi cha kwanza lakini sidhani kama atamaliza mchezo, najua ataelewa uamuzi huo, hawezi kuanzia benchi kwa sababu ni mchezaji mkubwa ambaye ana rekodi ya kipekee kwenye michuano hii na Ureno kwa jumla.

“Nafikiri hii ndio itakuwa njia rahisi kwake, pia sidhani kama atachezeshwa nafasi tofauti na ile aliyozoeleka kuichezea, naona atakuwa anaanza na kucheza kwa dakika kadhaa kisha atatoka.”

Fundi huyu anayemilikiwa na matajiri wa Saudia pia ndio mfungaji bora wa muda wote hadi sasa akiwa na mabao 14.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags