Rudeboy aendelea kutikisa, amnawa mwanasiasa Joe Igbokwe

Rudeboy aendelea kutikisa, amnawa mwanasiasa Joe Igbokwe

Mwanamuziki wa Nigeria Rudeboy amemnawa mwanasiasa kutoka chama cha ‘All Progressives Congress’ Joe Igbokwe kutokana na maoni yake kuhusu ugomvi kati ya msanii huyo na pacha wake, Peter Okoye, anayejulikana kama Mr P.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Rudeboy amemtolea povu mwanasiasa huyo kwa kumtaka awekeze nguvu zake kwenye siasa na kuacha kufuatilia mambo ya watu kwani wananchi wanakumbwa na janga la njaa hivyo ni bora akawasaidie.

Siku moja iliyopita mwanasiasa Joe Igbokwe kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika ujumbe akidai kuwa ameumizwa sana na kuona mapacha hao wameshindwa kuaminiana na kufanya kazi pamoja huku akiikashifu familia ya Okoye na wake wa wasanii hao kushindwa kuwasuluhisha mapacha hao waliowahi kutamba na ngoma ya ‘Taste The Money (Testimony)’.

Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa wiki iliyokwisha Paul Nonso Okoye ‘Rudeboy’ alithibitisha kuwa kundi la #PSquare limegawanyika kwa mara nyingine kwa kudai kuwa toka walivyoungana hakuna cha maana kilichowahi kufanyika.

Kundi P-Square lilisambaratika kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kuungana tena mwaka 2021, huku mwishoni mwa mwaka jana kukiwa na tetesi kuwa wawili hao wamegawanyika tena.
Wawili hao walitamba na ngoma zao kama ‘Taste The Money (Testimony )’, ‘Personally’, ‘Forever’ pia wamewahi kutoa ‘kolabo’ na mwanamuziki #Diamond wimbo uitwao ‘Kidogo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags