Saa ya abiria aliyezama meli ya Titanic yauzwa sh 3.7 bilioni

Saa ya abiria aliyezama meli ya Titanic yauzwa sh 3.7 bilioni

Saa ya mfukoni ya mfanyabiashara mkubwa aliyefariki dunia katika ajali ya meli ya Titanic, John Jacob Astor imepigwa mnada mara sita zaidi ya bei iliyokuwa ikiuzwa awali na kununuliwa kwa Dola za Marekani 146 milioni (Sh3.7 bilioni)

Imeripotiwa kuwa Astor alikuwa abiria tajiri zaidi kwenye meli hiyo iliyo zama na kuharibika vibaya mwaka 1912 na saa yake inaweza kufikia pauni 150,000.

Inaelezwa kuwa saa hiyo ya dhahabu ilipatikana wakati mwili wa Astor ulipotolewa kutoka bahari ya Atlantiki siku saba baada ya kuzama kwa meli hiyo iligonga jiwe la barafu katika safari yake ya kwanza kuelekea New York mwaka huo.

Hivyo mnada wa Andrew Aldridge unaeleza kuwa jumla ya gharama hii ni kama imevunja rekodi ya dunia ambapo saa hiyo ndiyo imeuzwa kwa pesa ya juu zaidi kuwahi kutokea kwa bidhaa moja iliyotokana na mali iliyoharibika kama meli ya Titanic.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags