Sababu wanaofariki wakiongeza makalio zatajwa

Sababu wanaofariki wakiongeza makalio zatajwa

Wataalamu bingwa wa upasuaji wa kurekebisha maumbile nchini, wametaja sababu tatu zinazoweza kusababisha anayepatiwa huduma ya kuongeza makalio kufariki dunia.

Sababu hizo zimetajwa kuwa ni hali ya kiafya ya mteja husika, utaalamu wa watoa huduma na mazingira yaliyopo wakati na baada ya upasuaji.

Ripoti ya upasuaji wa kurekebisha maumbile ya mwaka 2023 iliyofanywa nchini Marekani na tovuti ya ‘Research and Market’ inaonesha asilimia 42.7 ya waliofanyiwa upasuaji huo walipata madhara ikiwamo kifo.

Takwimu hizi zinaonyesha takribani nusu ya wote waliofanyiwa upasuaji wa kurekebisha maumbile hupata madhara hasi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags