Baada ya mwigizaji nguli wa Bollywood kutoka India Saif Ali Khan kufanyiwa upasuaji wa dharura baada ya kushambuliwa na jambazi na kuchomwa kisu, hatimaye madakatari wameweka wazi kuwa Saif ataruhusiwa hivi karibuni.
Utakumbuka kuwa mwigizaji huyo alivamiwa na jambazi nyumbani kwake Alhamisi Januari 16, 2025 na kujeruhiwa kwa kisu sehemu tofauti tofauti za mwili wake ikiwemo maeneo ya uti wa mgongo.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Peepingmoon’ kutoka India umeeleza kuwa daktari amefunguka kuwa Saif Ali Khan anatarajiwa kuruhusiwa kutoka hospitalini ndani ya siku mbili hadi tatu.
"Tunaendelea kufuatilia maendeleo yake, na kwa sasa anaendelea vizuri sana kulingana na matarajio yetu. Kwa mujibu wa maendeleo yake, tumemshauri apumzike kitandani, na ikiwa atahisi vizuri, basi ndani ya siku mbili hadi tatu tutamruhusu," alisema Dk. Nitin Dange siku ya Ijumaa.
Leave a Reply