Sanamu layeyuka kisa joto kali

Sanamu layeyuka kisa joto kali

Sanamu la aliyewahi kuwa rais wa Marekani na mwanasheria Abraham Lincoln lililopo Washington DC, limeripotiwa kuyeyuka huku sababu ikitajwa ni joto kali nchini humo ambapo mpaka kufikia sasa lishafikia nyuzi joto 100.

Sanamu hilo lenye futi sita lililotengenezwa na Sandy Williams IV kama sehemu ya ‘The Wax Monument Series’ liliwekwa katika shule ya Msingi ya ‘Garrison’ Februari mwaka huu limezua gumzo mitandaoni baada ya kuyeyuka na kupelekea shingo kuvunjika.

Joto kali nchini humo limekuwa janga ambalo lisiloepukika kwani wakazi wa nchi hiyo wamekuwa wakihofia usalama wa maisha yao endapo nyuzi joto ikiendelea kuongezeka zaidi.

Utakumbuka siku moja iliyopita mwamuziki msaidiza Humberto Panjoj katika ‘mechi’ ya Peru na Canada alidondoka uwanjani kutokana na kuzidiwa na joto kali, hali iliyopelekea mpaka wachezaji wa ‘timu’ nyingine kuhofia usalama wao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags