Sancho aendelea kushushiwa adhabu

Sancho aendelea kushushiwa adhabu

Baada ya mchezaji maarufu kutoka’ klabu’ ya Manchester United, Jadon Sancho kuzuiliwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza siku chache zilizopita, ‘timu’ hiyo imezuia tena mchezaji huyo kutumia vifaa vya kufanyia mazoezi alivyokuwa akivitumia awali.

Hii inakuja baada ya kupewa adhabu na kudaiwa kuwa na migogoro na ‘kocha’ Erik Ten Hag huku akipewa sharti la kumuomba radhi ‘kocha’ huyo jambo ambalo hajalitekeleza mpaka sasa.

Sancho tangu aondolewe kwenye kikosi amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha vijana hata wakati wa kula hatakiwi kutumia sehemu ya chakula wanayotumia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags