Savanna: Familia yangu iligoma kunihudumia kisa mitandao

Savanna: Familia yangu iligoma kunihudumia kisa mitandao

Na Aisha Charles

Katika kutafuta njia ya kupambania ndoto zako ukiwa chini ya uangalizi wa wazazi hasa ukiwa unawategemea kwa kila kitu lazima kutakuwa na mashaka, mzazi au mlezi hofu yake huwa inakuja pale anapojiuliza kuwa kama utaweza kupambania ndoto zako kupitia njia uliyoichagua.

Muda mwingine mashaka ya wazazi hasa wa Kiafrika yanaweza kakufanya ukaishi kupitia ndoto zao na sio ndoto zako binafsi, lakini kitu wasichokijua kwamba zama zimebadilika kutokana na utandawazi.

Mwananchi Scoop, ilibisha hodi hadi kwa mwanafunzi kutoka Chuo cha Maji ,Dar es Salaam, Savanna Benson maarufu kama Rais wa First Year ambaye ni Contents Creator wa mitandao ya kijamii hasa Tiktok,amesimulia kuwa wakati anaanza kujikita na mitandao ya kijamii wazazi wake walimkataza kwa kuhofia usalama wake.

“Kama kawaida kwenye kufanya jambo fulani lazima mzazi awe na hofu kuhusu usalama wako kwa sababu watu walikuwa wanafikiria nitaingia kwenye makundi mabaya na ilikuwa ngumu kwao kukubaliana na mimi.”

Wazazi wangu walisitisha kunihudumia baadhi ya vitu

Kuna msemo unasema ili upate kitu lazima uharibu kitu ndivyo ilivyokuwa kwa Savanna ambapo amedai kuwa kutokana na kung’ang’ania msimamo wake wa ku-deal na mitandao kwa kutengeneza contents wazazi wake walisitisha baadhi ya huduma na kumuacha ajitegemee mwenyewe.

“Wazazi wangu walinambia kama naendelea kufanya hivyo itabidi wapunguze kufanya baadhi ya vitu kutoka kwangu na nilikuwa tayari kwa hilo, kwa sababu yale majukumu ambayo walinipa wakati ule bado naendelea nayo mpaka sasa na ndiyo chaguo nliloliamua ingawa sasa kidogo wako sawa lakini mwanzo ilikuwa mbaya zaidi” amesema.

Familia ilivyo mtafutia mshauri yangu aachane na mitandao

Haikuwa rahisi kwa Savanna kuwashawishi wazazi bado waliendelea na msimamo huohuo hadi kufika hatua ya kumtafutia mshauri ambaye alikuwa ni shangazi yake lakini haikufua dafu.

“Kuna kipindi walijitahidi hadi kunitafutia mshauri ambaye angeweza kuongea na mimi niachane na mitandao ya kijamii ambaye alikuwa Aunt yangu lakini ikashindikana hadi hivi leo kwa sababu nilikuwa na ndoto ya kuwa mwana Social Media,”anasimulia.

 

Faida anayoipata kupitia mitandao ya kijamii

 

Savanna ameleeza faida anayoipata kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo kupata pesa ya kujikwamua katika maisha yake na imemkutanisha na watu maarufu ambapo awali hakuwahi kukutana nao labda kuwaona kwenye runinga kama Ali Kiba na Nandy.

“Kwanza nikupata pesa kuweza kujikimu mwenyewe, nime-gain popularity ambayo itani-fever some places kwenye maisha, imenikutanisha na watu ambao sjawahi kukutana nao awali nlikuwa nawaona tu kwenye TV kwa sababu nlishawahi kwenda kwenye event ya Ali Kiba na Nandy ambayo walialika Tiktoker wote,” amesema.

Pia ameongeza kuwa kukutana na watu tofauti tena maarufu imemsaidia sana na hakufikiria kufika sehemu ambazo mpaka sasa amefika kupitia social media.

Anatengenezaje pesa kupitia mitandao?

Hata hivyo, amefunguka jinsi anavyotengeneza pesa kupitia mitandao ya kijamii ambapo amesema kupitia matangazo na live za TikTok ndiyo imemfanya kupata pesa.

“Natengeneza pesa kupitia matangazo kwa sababu some of people huwa wanataka niwe ‘Nawatangazia bidhaa zao mtandaoni kingine zile live za TikTok nikienda na piga zangu stori kuna zile gift wazozituma unaweza kubadilisha kuwa pesa,” anasema.

Aidha ameeleza kiasi cha pesa ambacho anapata kupitia mitandao ni kikubwa na kinaweza kumpa mafanikio makubwa kama kununua gari na mambo mengine.

“Kiasi cha pesa ninachopata kupitia mitandao kama nilivyosema awali kinanisaidia kujikimu maisha kwa sababu ni kikubwa na kama ukiji-make unaweza kununua gari na mambo mengine, hatuwezi kuwa tunafanya kazi na makampuni makubwa tushindwe kulipwa hela nzuri kwa hiyo ukiacha kuwa na majina na kazi yetu inaonekana,” amesema.

Hadhari anazozipata katika masomo kupitia umaarufu wake

Kama tujuavyo kila kitu kina faida na hasara, Savanna amesimulia akiwa bado Mwanafunzi kuna muda anapata athari kwa sababu ya umaarufu wake ambapo kuna muda anakuwa yupo katika masomo anashindwa ku-post contents zake mtandaoni hali inayomfanya apoteze audience wake.

“Kuna muda napata athari kupitia umaarufu wangu, kuna muda nashindwa ku-post contents kwa sababu ya masomo pia nashindwa ku create contents kwa mfano msimu wa UE chuoni nakuwa busy sana na nasahau kabisa kama nina mitandao ya kijamii jambo ambalo linaweza kunirudisha nyuma na niki-focus na mitandao ya kijamii sana naweza nikapitwa na vitu chuoni lakini najitahidi ku-balance,” anasema Savanna.

Alivyoona ndoto zake za kuwa staa kabla hajaingia katika mitandao

Savanna amedai kuwa alikuwa anaziona ndoto zake za kuwa staa kabla ya kujihusisha katika mitandao ya kijamii kwa sababu alikuwa Topic shuleni hivyo alifikia kuwa akiwa mkubwa atatumia uwezo wake kuwa staa.

“Kabla ya kujihusisha na mitandao nlikuwa naona nimezaliwa kuwa staa, kwa sababu nilikuwa Topic sana hivyo nikawaza nikiwa mkubwa nitatumia mdomo wangu kitu ambacho nakifikiria watu wengi huwa wananiambia niliwaza nini kufanya vitu ambavyo vinatrend sasa kupitia mitandao ya kijamii,” amesema.

Mbali na hayo, Savanna ameeleza kuwa hajutii kujihusisha katika mitandao ya kijamii bali anaona ametimiza ndoto yake.

Pia ameongezea kwa kuwashauri watu wanaoandaa contents kupitia mitandao ya kijamii kwa kuwashauri kuwa kufanya Contents kunahitaji ubunifu na waache kuvuma mitandaoni bila kuwa na maudhui yanayoeleweka hiyo itawaumiza baadaye na kuwataka wawe wavumilifu kama wanataka kuwa mastaa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post