Sean: Kitendo cha Will Smith kumpiga Chris Rock alitakiwa kwenda jela

Sean: Kitendo cha Will Smith kumpiga Chris Rock alitakiwa kwenda jela

Mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani Sean Penn, akumbushia tukio la Will Smith kumpiga kofi Chris Rock baada ya kumfanyia masihara mke wake.

Sean akiwa katika mahojiano nchini humo amedai kuwa Will alitakiwa kwenda jela baada ya kumpiga Chris katika usiku wa Tuzo za Oscar mwaka 2022.

Muigizaji huo mkongwe amedai kuwa amekuwa akijiuliza ni kwanini Will hakwenda jela kwa tukio hilo?, kwani hata yeye  mwaka 1987  akiwa na umri wa miaka 26 aliwahi kumpiga ngumu mtu na matokeo yake alipelekwa gerezani kwa siku 60 na kutumikia kifungo kwa siku 33, jambo ambalo limekuwa tofauti kwa Will.

Sean Penn amecheza filamu kama vile “I am Sam” (2001), “into the wild” (2007), “Milk” (2008), “Mystic river” (2003) na nyingine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags