‘Rapa’ Snoop Dogg ameripotiwa kuja na muendelezo wa kipindi cha watoto kilichopewa jina la ‘Doggland’ ambacho kitasaidia watoto kujifunza vitu mbalimbali, kama vile kuimba, kucheza, na kuelimisha, kipindi hicho kitakachoruka katika mtandao wa ‘YouTube Kids’ kitakachoruka kila wiki.
Dogg akishirikiana na mtayarishaji Claude Brooks pamoja na mwanamuziki Oktoba London, yeye ndiye anayetoa sauti ya muhusika mkuu ambapo watoto wataweza kujifunza muziki wa densi, watafundishwa ujuzi wa kijamii na hisia katika kutambua vitu.
Snoop kufuatiwa na mahojiano yake ameeleza kuwa kujitolea kwake kuunda maudhui chanya kwa watoto yanakuja kutokana ana uzoefu wake kama baba, babu na ‘kocha’ wa soka la vijana.
Leave a Reply