Mwaka 2024 umekuwa mgumu kwa kampuni ya Sony Pictures, hasa katika mauzo ya filamu zake tatu ikiwa ni pamoja na Kraven the Hunter, Venom: The Last Dance, na Madame Web, baada ya kufanya vibaya sokoni.
Kutokana na hilo tetesi zinazodai kuwa Sony inafikiria kuuza haki miliki za filamu ya Spider-Man kwa Marvel Studios.
Utakumbuka awali Sony ilianzisha ushirikiano na Marvel Studios mwaka 2016, na Spider-Man alionekana kuunganishwa rasmi na Marvel Cinematic Universe (MCU) kupitia filamu Captain America: Civil War.
Ushirikiano huo ulikuwa hatua kubwa kwa waigizaji wa filamu ya Spider-Man, Spider-Man: Homecoming, Spider-Man: Far From Home, na Spider-Man: No Way Home hasa kwa Tom Holland, ambaye alicheza kama Spider-Man.
Baada ya hapo Sony ilijaribu kuzindua filamu zake za muundo mpya kama Venom na Morbius, ambazo zilipata mafanikio kidogo, na baadhi ya filamu zilizofuata hazikufanya vizuri kabisa kibiashara.

Leave a Reply