Taylor Swift ameza mdudu, Ashindwa kuendelea na show

Taylor Swift ameza mdudu, Ashindwa kuendelea na show

Mwanamuziki wa Marekani #TaylorSwift amedaiwa kumeza mdudu na kushindwa kuendelea na show katika ziara yake ya dunia ya Eras iliyofanyika jijini London nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Page Six News’ imeeleza kuwa Taylor alimeza mdudu kwa bahati mbaya wakati akiimba wimbo wake wa ‘All Too Well’ jambo ambalo lilipelekea kushindwa kuendelea na kuimba kwa muda.

Taylor mwenye umri wa miak 34 baada ya kupata kikohozi cha ghafla alishindwa kuendelea kutumbuiza na kuwatangazia mashabiki zake kuwa amemeza mdudu, hivyo aliwaambia waendelee kuimba wenyewe.

Hii siyo mara ya kwanza kwa msanii huyo kukutana na tukio kama hilo mwaka jana nyota huyo wa Pop aliwahi kupata kikohozi cha ghafla wakati akitumbuiza katika ukumbi wa Solder Fiel huko Chicago.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags