Teknolojia inavyosaidia malezi ya watoto

Teknolojia inavyosaidia malezi ya watoto

Uwepo wa mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia kumechangia mambo mengi sana kukua kwa kasi hapa duniani, nafikiri hili limedhihirika hata kwako wewe ambaye unasoma makala haya au nadanganya?

Twende sawa basi mshikaji wangu wa faida mwana mwenyewe, yani hivi unafahamu kuwa leo ni siku ya Mtoto wa Afrika Duniani ambayo huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu na umuhimu wa mtoto kwenye jamii.

Always maadhimisho haya hufanyika kila Juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na Jumuiya ya Umoja wa Afrika, nimekuandalia makala ambayo itaangazia zaidi maendeleo haya yameleta mabadiliko chanya kiasi gani kwa watoto wetu.

Kauli mbiu ya Maadhimisho haya ni “Mtoto ni Msingi wa Taifa Endelevu Tumtunze, Tumlinde na Kumuendeleza”

  1. Breastfeeding pump

Wakati watu wakihangaika namna ya kumnyonyesha mtoto, teknolojia imetuletea kitu kipya, nayo ni pump ya maziwa.

Sasa unaweza kuweka maziwa ya mama kwenye chupa kupitia pump na kuhakikisha kuwa mtoto wako atakunywa maziwa ya mama hata pale ambapo hautakuwepo. Cha msingi tu ni kuzingatia kuyatunza maziwa hayo sehemu salama ili yasiharibike.

  1. Baby troller

Ukienda kwenye Malls au sehemu fancy na kukutana na mama mwenye mtoto, bila shaka atakuwa na troller pemebeni. You don’t have to always hold your baby kwa kuwa unaweza kuchoka, kuwa na baby troller inasaidia sana kuweka mtoto mahala salama na kuzunguka nae bila ya wewe kuchoka. Kweli tech ni kiboko yao.

  1. Baby Monitor

Sasa kama wewe ni wale independent mothers na unapenda kufanya mambo yako mengine hata ukiwa na mtoto, this one is to look out for. A baby monitor inakusaidia kuweza kumuangalia na kumsikia mwanao hata ukiwa kwenye chumba kingine, hivyo kama akilia tu au akiamka, utaweza kumsikia na kumuona. Hii inarahisisha sana katika parenting kwani na wewe mzazi utapata uhuru wa muda bila ya kuwazia kama mtoto wako yupo salama.

  1. RockaRoo by 4moms

Hii ni kifaa maalum kinachoweza kumbembeleza mwanao kwa kumswing huku na kule. Ni kifaa kizuri sana kama mwanao anapenda kubebwa bebwa kwani atajihisi yupo katika bembea na kwenye suala la kulala, litakuwa limeisha hivyo. Kweli teknolojia inafanya maisha ya kuwa mama yanakuwa ni no stress. Kudos kwa uvumbuzi huu akiii.

  1. Baby Shusher

Je mwanao ni msumbufu halafu unatamani kulia kwa kumbembeleza? Basi technology imekuletea suluhisho.

Baby Shusher ni kifaa ambacho kinaweza kum-calm down mwanao hadi akaomba poo. Kifaa hicho kitambembeleza mwanao kwa muda wa dakika 15-30 huku kikitembea huku na kule, yaani dogo hapo asipobloo, ndo basi tena!

  1. Baby dam

Ule wakati wa kuwaogeshea watoto ndani ya mabeseni umepitwa na wakati. Sasa technology inakuletea mambo mapyaaa kabisa.

Baby dam ni kifaa ambacho kipo kama beseni, lakini inaweza kuzuia mwanao kutoanguka wakati wa kuoga, vile vile utaweza kumuwekea toys wakati anaoga na hata distance kati yako na mwanao haitokuwa kubwa, hivyo itakusaidia wewe kuweza kumuogesha mwanao bila wasiwasi wowote ule.

  1. Sleep training alarm clock

Waswahili tushazoea zetu kuwa alarm ni ya kukuamsha tu, lakini wapiiii!

Hii alarm ni maalumu kwaajili ya kumfundisha mtoto muda wa kulala, hivyo unaiset kwa muda tofauti tofauti katika siku, na yenyewe itamuwezesha mwanao kuzoea muda wa kulala na kuamka kila siku. Mambo hayo.

  1. Magnetic high chair

Kama mwanao ndo kama watoto wa kina sie basi hili nalo linakuhusu shoo...

Ni hivi, kuna wale watoto wasiopenda kabisa kula, sasa dawa yao teknolojia inayo. Hiki kiti ukiwa nacho yaani hauna hata haja ya kubana mtoto miguu, ni atakula tu. Kwanza kitu kipo juu, unaweza kumlisha huku umesimama, na kinambana mtoto vizuri kiasi kwamba hafurukuti. Sasa kama mwanao alijikuta mjanja, mbele ya hiki kiti ndo atajua hajui.

Kuna vitu vingi sana vya kuwasaidia wazazi waweze kuwalea watoto wao katika modern standard. Maisha yamerahisihwa sana kipindi hiki kwasababu ya teknolojia. Honestly, najua mengine mengi yatavumbuliwa, hivyo to us future moms, lets watch out!

Waow this is how Technology inavyofanya kazi katika Nyanja zote, how happy it is my friend? Always kuwepo kwa mabadiliko na mafanikio ya kasi duniani hakika yameletwa na mapinduzi makubwa ya Science na Techology let people lives in Technology lifeeeee!!!!!!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags