Ten Hag akiondoka Sancho anarudi United

Ten Hag akiondoka Sancho anarudi United

Mchezaji wa zamani wa ‘klabu’ ya Manchester United, Jadon Sancho ambaye kwasasa anakipiga Borussia Dortmund ameripotiwa kueleza kuwa yupo tayari kurudi Man United endapo meneja wa ‘timu’ hiyo Erik Ten Hag ataondoka klabuni hapo.

Wawili hao hawakuwa na mahusiano mazuri ndani ya klabu ambapo walihusishwa katika migogoro kadhaa iliyopelekea mchezaji huyo kuondolewa kikosi cha kwanza pamoja na group la WhatsApp la ‘timu’ hiyo.

Jadon Sancho alijiunga tena na ‘klabu’ yake ya zamani ya Borussia Dortmund Januari mwaka huu akienda huko kwa mkopo ambapo ataitumikia ‘timu’ hiyo hadi mwisho wa msimu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags