Tips zitazokusaidia kujitafuta mapema

Tips zitazokusaidia kujitafuta mapema

Oyaaaah! Wanangu, majobless tuwaambie hawa watu au tuwaache kidogo waone joto la jiwe hahaha!, Lakini wacha tuwajuze wasije kujuta baadae. Haya sasa leo katika segment yetu ile ile ya mada za wanavyuo, tumekusogezea topic ambayo ukiisoma na kuielewa basi utakuwa umetoboa sana.

Mara nyingi huwa tunatamani kujitambua na tunasikia watu wengi wakituambia umuhimu wa kujitafuta na kujitambua, lakini kama wewe umepitia hali ninayopitia mimi basi umejiuliza sana, nawezaje kujitafuta?

Kama upo kwenye kipindi cha kujiuliza hivyo naomba nikuambie njia kadhaa ambazo zimenisaidia mimi na baadhi ya watu kujitafuta, ambazo na uhakika zinaweza zikukusaidia na wewe pia.

Kujitafuta ni kitendo kinachochukua muda, sio jambo la mara moja kwahiyo usijihisi una mapungufu mengi ambayo hauwezi kuyafanyia kazi au usijihisi safari ni ndefu hauna haja ya kuianza, kujijua wewe mwenyewe ndio raha ya maisha maana wewe mwenyewe ndio utaishi maisha yako na wewe kila siku, ni vizuri ukijijua.

Kuna baadhi ya watu walikuwa wananambia kuwa maisha yao waliyawaza na kuyatengeneza tangu walipo maliza shule, sikuwaelewa lakini nimekuja kuelewa baada ya mimi kuamua kusimamia maisha yangu mwenyewe na kuyapanga yawaje.

Njia zitakazo kusaidia ili uweze kujitambua…

  • Kujisikiliza

Utashangaa ni mara ngapi huwa hatujisikilizi. Ni mara ngapi maamuzi, au maisha tunayoishi tunafanya kwaajili ya wengine. Hata leo tu jiulize umetumia muda gani kutulia na kusikiliza jinsi unavyojisikia au kitu unachokitaka, ni mara ngapi? Njia rahisi ya kujijua wewe, ni kujisikiliza wewe pia. Penda sana kusikiliza moyo wako hasa katika kufanya maamuzi, skiliza sana moyo wako, ukisema jambo hili usilifanye basi usifanye na ukisema jambo hili fanya basi fanya.

Wacha niwaibie siri hata katika mahusiano yako sikiliza moyo wako usipende kusikiliza watu wanasema nini, zingatia hili utakuja kunishukuru baadae, usipende kusikiliza sana watu hakuna anaependa mafanikio yako.

  • Kujiuliza maswali

Kujiuliza maswali magumu na kukaa chini kusikiliza majibu uliyonayo, na kwanini unayohayo majibu uliyonayo.

Katika maisha ya sasa hivi rahisi kuwa mfuata njia na sio mfikiriaji mwenyewe, ukijiuliza maswali utajijua vizuri, utajua msimamo wako kuhusu mambo fulani nk. Na hii sio lazima ujiulize mchana unaweza kujiuliza kabla haujalala yaani ukiwa kitandani usiku unachangamsha ubongo.

  • kusoma vitabu

Nakumbuka kuna kitabu kimoja ambacho nilisoma kiliniliza sana na nikagundua kuhusu jambo ninalolipenda kupitia hicho kitabu maana nilikuwa sijui kama moyo wangu unaguswa katika eneo hilo.

Vitabu vinakufungulia dunia na mawazo mapya, na kukufanya uone mbali ya zaidi ulipo, lakini pia kwa kuona mbali, unaona na karibu pia, unajiona ndani ya moyo wako.

Nafikiri kuna baadhi ya watu watanielewa nini namaanisha kuna ile feeling unapofanya jambo unajiona kabisa unaamani na umeshatoboa kimaisha.

  • Kujaribu kufanya vitu vipya mbalimbali

Unapofanya vitu mbalimbali unajifunza na kujijua zaidi, kipi unaweza, kipi hauwezi, kipi unapenda, wapi uko vizuri, kipi kinakukasirisha, kwanini kinakukasirisha nk. So jitahidi kuchakarika mambo mbalimbali ndo mana tunaambiwa tusisome kozi moja inabidi tuchangamshe ubongo kwa kufanya hayo utajipata na kufanikiwa mapema tuuh.

 

  • Kuwauliza watu kuhusu wewe

Kuwauliza watu wanakuonaje au kukufikiriaje hasa watu unaojua wana nia nzuri na wewe.

Kuna mtu alinifundisha kitu, alisema kuna mambo manne dunia;

  • Mambo unayoyajua kuhusu wewe lakini watu wanayajua
  • Mambo unayoyajua kuhusu wewe ila watu hawajui
  • Mambo usiyoyajua kuhusu wewe ila watu wanayajua
  • Mambo usiyoyajua kuhusu wewe na watu hawayajui

Kuwauliza watu wanaokujua vizuri wanaweza kukusaidia kujua mambo usiyoyajua kuhusu wewe ambayo wao wanayajua kwa kukuangalia labda au kwa kufahamu na kuona ubora wako.

  • Kujifunza kutoka kwa wengine

Kwa kuwa hakuna jipya chini ya jua, sio vibaya ukipenda kitu kwa mtu ukajifunza kutoka kwake na pia ukakichukua. Hiki pia kinaweza kuwa kipimo cha kujitambua kwako kwa kuangalia mambo unayojifunza kutoka kwa wengine.

  • Kumuomba Mungu

Njia na jambo la muhimu kabisa ni kumuomba Mungu, Yeye aliyekuumba anakujua vizuri. Kwahiyo unapojitafuta ukimuomba na kumsikiliza Yeye ni rahisi sana kujijua. Inabidi uache wakati wa mungu uamue usiforce mambo kuna msemo unasema kama ni yako basi itakuwa tuu hata wengine wafanyaje lazima itakuwa tuuu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags