Mkali wa Afrobeat nchini Nigeria Tiwa Savage ameeleza kujutia kuachana na mume wake na kuanzisha uhusiano na mwanaume mwingine.
Akizungumza kwenye mahojiano yake na moja ya chombo cha habari nchini humo amesema anajutia uamuzi huo.
"Nilimfanya mume wangu asijisikie kuwa mwanaume kwa sababu nilianza kutoka na mwanaume mwingine, bado nampenda mume wangu na najua nilimkosea lakini nataka kurekebisha mambo na kurudiana.
"Sina uhakika kuwa anaweza kunirudisha tena, samahani kwa kumuacha mume wangu, sikuwahi kutaka kumpa talaka lakini mwanaume mwingine alinihadaa nimuache mume wangu na nadhani nini.
Sio rahisi kuoa mwanamke aliyemwacha mumewe kwa mwanamume mwingine,”amesema Tiwa
Mbali na hilo nyota huyo wa muziki amewasihi wanawake kutofanya alichokifanya kwani kitawafanya wajutie maisha yao yote.
“Bado nampenda mume wangu na ninajutia kila nililomfanyia. Nadhani niliacha umaarufu na pesa ziingie kichwani mwangu lakini sasa kwa kuwa nimekuwa mkubwa nimegundua kwamba mambo haya hayana umuhimu wowote. Nataka apate nafuu. Sisemi hili kwa kamera, ni kutoka moyoni mwangu.
"Wanawake wapendwa, usimwache mumeo kwa mwanaume mwingine au utaenda kujuta maisha yako yote. Laiti ningelijua hili mapema, nisingekuwa katika nafasi hii,” amemalizia Tiwa Savage
Ikumbukwe kuwa Tiwa Savage aliwahi kufunga ndoa na Tunji maarufu ‘Tee Billz’ Balogun mwaka 2013 na kutengana mwaka 2016 baada ya kidanganywa na mwanaume mwenye fedha ambaye hajafahamika jina lake. Wawili hao walijaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jamil Balogun.
Leave a Reply