Tory Lanez na selo ya peke yake

Tory Lanez na selo ya peke yake

Baada ya purukushani za ‘kesi’ ya ‘rapa’ kutoka Marekani, Tory Lanez kuisha siku kadhaa na hatimaye kupelekwa gerezani rasmi, inadaiwa kuwa mfungwa huyo anaishi ‘selo’ ya peke yake.

Kwa mujibu wa TMZ news imeeleza kuwa rapper huyo ametengwa katika ‘selo’ ya peke yake kwa sababu ya kuwa mtu maarufu, na inasemekana kuwa anatumia choo cha peke yake na hata chakula anapelekewa katika chumba chake na inaelezwa kuwa hukaguliwa mara kwa mara na walinzi.

Ikumbukwe kuwa Tory alipelekwa gerezani siku ya Jumanne baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 kwa kukutwa na hatia katika kesi ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags