Tyla Tena Tuzo Za Billborad 2024

Tyla Tena Tuzo Za Billborad 2024

Na Asma Hamis

Mwanamuziki kutoka Afrika Kusini ambaye alitamba na wimbo wa ‘Water’ Tyla ameendelea kung’ara Kimataifa na sasa ameripotiwa kushindwa tuzo ya msanii bora katika tuzo za Billboard Music 2024.

Kwa mujibu wa tovuti ya Billboard imeweka wazi kwamba Nyimbo yake ya Water, Truth or Dare na Jump kutoka kwenye albamu yake ya kwanza iliyoipa jina lake (Tyla) zilikamata chati Billboard 200 mfululizo na kumpelekea kuondoka na tuzo mbili ikiwemo Top Afrobeats Artist na Top Afrobeats Song.

Haya si mafanikio ya kwanza kwa Tyla kuyapata kwa mwaka huu kwani kupiti wimbo wa ‘Water’ amenyakuwa tuzo ya Grammy katika kipengele cha Best African Music Performance, Best Afrobeats at the 2024 Video Music Awards na nyinginezo.

Hata hivyo Tyla hakuwa nyota pekee aliyeshinda tuzo hizo wapo mastaa wengine akiwemo Tylor Swift, Drake, Bruno Mars, Doja Cat, Travis Scott, Beyoncé, na wengineo wengi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags