Hili ndilo limetokea kwa mwalimu wa mpira wa miguu. Ambaye kwa miongo miwili hii. Soka la ngazi za vilabu duniani, kaliteka na kuliweka chini ya soksi zake.
Pep Guardiola kakamilisha talaka yake kwa mkewe. Katika talaka hiyo, kapoteza jumba lake kubwa zaidi la kifahari huko Manchester. Dunia ya wenzetu noma sana.
Ukiachana na jumba hilo, nusu ya utajiri wake na mali zake nyingi. Zikienda kwenye mamlaka ya mtalaka wake huyo na watoto. Uso wa dunia upo na mwanamke.
Tunakumbushwa kuishi kwa akili na wanawake. Mke wa Pep katika madai yake, alilalamika kuwa Pep alizingatia zaidi soka na hakuwa na muda na familia yake.
Wakati kina Mwajei na kina Stellah huko Bonyokwa na Kijiwe Samri ya Kiwalani, wakiwaza pesa zaidi. Mke wa Pep aliutaka muda wa Pep na siyo pesa za Pep. Hii dunia bana.
Pep ni kocha maarufu duniani na tajiri wa kipato. Pesa na umaarufu wake siyo kitu mbele ya mtalaka wake. Bi dada alitaka muda wake, maana pesa zipo.
Pep aliondoka mahakamani akilia. Chozi likimtoka kama la mashabiki wa Madrid. Alipotoa kipigo cha goli tano pale Bernabéu miaka kadhaa nyuma. Akiwa na 'Wakatalunya'.
Sasa anapambana na wakati huu mgumu. Wakati huu mgumu familia yake ikimtenga, wakati huu mgumu timu yake kufanya vibaya kwenye ligi. Wanawake tuishi nao kwa akili
Leave a Reply