Inafahamika dharula kwenye maisha ya mwanadamu ni kitu ambacho hakiepukiki. Kutokana na kukwama au kupitia changamoto kuna umuhimu mkubwa kwa bosi au msimamizi kuelewa dharula za wafanyakazi ili kujenga mazingira mazuri ya kazi. Faida za boss kuelewa watu anao wasimamia
- Kujenga mahusiano mazuri, bosi anayeelewa dharula za wafanyakazi huonyesha huruma na kujali. Jambo hili husaidia kujenga uaminifu na mahusiano mazuri kazini baina yake na wafanyakazi.
2.Huongeza morali ya wafanyakazi, wafanyakazi wakihisi kueleweka, wanakuwa na motisha zaidi kufanya kazi kwa bidii kwa sababu wanaelewa imani waliyopewa na ofisi na hivyo hawakubali kuivunja licha ya kupitia changamoto.
3.Kuhamasisha uaminifu, wafanyakazi wanaotendewa haki na kueleweka wanakuwa waaminifu kwa kampuni na huchangia kwa ufanisi mkubwa. Hii pia husadia mfanyakazi kujiona yupo sehemu sahihi kwa sababu anaaminika licha ya kupitia changamoto ambazo zinapelekea dharula yake.
4.Hupunguza msongo wa mawazo, ukiwa na boss anayeelewa dharula husaidia wafanyakazi kupunguza msongo wa mawazo wanapokumbwa na changamoto za kazi na hata za kibinafsi, kwani huelewa kwamba suala analopitia bosi au msimamizi atamuelewa na kumpa muda wakukamilisha zoezi hilo.
5.Huimarisha utendaji kazi, wafanyakazi wanaojua boss au msimamizi wao ni muelewa linapokuja suala la dharula au changamoto ya kazi, wanarudi kazini wakiwa na nguvu mpya. Hivyo huongeza uzalishaji kwa sababu hutamani kuonesha weledi ambao wako nao licha ya kupitia changamoto na vizuizi.
6.Hujenga utamaduni wa heshima, inasaidia kujenga utamaduni wa heshima na mawasiliano mazuri ndani ya shirika, ofisi, kampuni au sehemu yoyote ya kazi kwa sababu wafanyakazi wanakuwa wanaelewana na uongozi hivyo heshima inatawala zaidi.
7.Kuzuia ufukuzwaji na uhamaji wa wafanyakazi, Wafanyakazi wanaohisi kueleweka na kuthaminiwa huwa na uwezekano mdogo wa kutafuta kazi sehemu nyingine au kufukuzwa kazi kabisa. Kwani boss akimuelewa mfanyakazi hatochukua maamuzi ya kumfukuza na mfanyakazi akieleweka ataona anathanika na kutochukua maamuzi ya kutafuta kazi nyingine au kujihisi tofauti.
Leave a Reply