Utunzaji wa ngozi kwa wanaume

Utunzaji wa ngozi kwa wanaume

Aisha Charles

Hello guys! acha nikusalimu kwa jina la fashion. Leo tumeingia kwa undani zaidi katika masuala ya urembo, tumekusogezea jinsi ya kutunza ngozi kwa wanaume.

Hivi unajua muonekano mzuri unaanzia kwenye ngozi, wengi hawafahamu suala hali hasa kwa wanaume wamekuwa ni watu wasiojali ngozi zao.

 Ngozi ya mwanadamu ni sehemu ya mwili ambayo inahitaji matunzo kama zilivyo sehemu nyingine.

Tofauti na hapo mtu asipotunza ngozi yake inaweza kufanya akapoteza mvuto na kupata magonjwa ya ngozi kama vile chunusi, mapele ukurutu na mengineyo.

Kumekuwa na dhana mbalimbali kwa jamii, kuhusiana na utunzaji wa ngozi wengi wanadhani utunzaji wa ngozi ni kwa wanawake tu.

 Hilo linadhihirishwa na Albert Changarawe mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam ambaye anasema afahamu njia yoyote ya kutunza ngozi yake zaidi ya kuoga kwa maji safi pamoja na kupaka mafuta.

“Hayo masuala mara nyingi hufanywa na wanawake kwa sababu ndiyo wanapenda urembo” alinasema Albert.

Hata hivyo kwa upande wa Hassan Hassan mkazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam anasema imezoeleka katika jamii kuwa suala la kutunza ngozi ni mwanamke pekee.

“Mara nyingi baadhi ya wanaume hufanya uamuzi wa kuanza kuzitunza ngozi zao hadi pale wanapopata changamoto ya ngozi kama vile kuwashwa, kupata mapele na nyinginezo”alinasema kijana huyo.

Hata hivyo wataalamu wa masuala ya ngozi na urembo wanaeleza kuwa wanaume wana wajibu wa kujijali katika sekta zote za urembo na

fashion katika masuala ya utunzaji wa ngozi zao kama wanavyofanya wanawake kwani muonekano mzuri usoni kwa wanaume husababishwa na kujali vizuri ngozi na uso kwa ujumla.

Akizungumza na Mwananchi Scoop mtaalamu wa masuala ya urembo na fashion kutoka Crystal Wedding Accessories, Irene Shamge anasema  ili mwanaume aweze kuwa na ngozi nzuri anapaswa kuwa na tabia ya kunawa uso mara kwa mara ili kuondoa takataka, vumbi pamoja na jasho lililoingia katika ngozi kutokana na mizunguko ya siku nzima.

“Vumbi, jasho na hata takataka zingine katika ngozi haswa ya uso zikikaa kwa muda mrefu huweza kusababisha changamoto ya kupata chunusi, mapele na hata kuharibika kwa ngozi na hauwezi kwenda na fashion” alinasema mwanamitindo huyo.

Irene anasema matumizi ya visafisha uso (facial cleanser) kila asubuhi ni muhimu pia kwa wanaume kwani husaidia ngozi zao kutoa uchafu na mafuta yaliyozidi kwenye ngozi na kuacha ngozi ikiwa nzuri kabisa.

Pia kufanya singo (scrub) mara moja au mbili kwa wiki itasaidia kuondoa seli zilizokufa kwenye ngozi na kuifanya kuwa yenye kuvutia na huleta muonekano mzuri.

“Pia baada ya kunyoa ndevu ni vyema kutumia mafuta yatakayosaidia kuepusha na kupata vipele, kwa wale wanaofuga kwa ajili ya fashion ni vizuri kuzitunza ili kuweza kuwa na muonekano mzuri” alisema Irene.

Vilevile anasema ni muhimu kutumia mafuta au losheni inayoendana na ngozi ya mwili  ili kulainisha ngozi.

Anaongezea kuwa ni muhimu kunywa maji ya kutosha kwani husaidia kuzuia kuondoa uchafu na mabaki ya uchafu mwilini kwa njia ya jasho na mkojo pamoja na kupunguza uchovu wa mwili.

“Mtu mzima anashauriwa kunywa maji safi na salama kiasi cha lita moja na nusu kwa siku au glasi nane kwa siku”

Nikikwambiaga fashion imebeba vitu vingi ni maisha ya kila siku kama kwenye afya, urembo na muonekano mzuri hapa hauwezi ukabisha mwanetu muonekano wa mtu unazingatia hadi mtindo wake wa kawaida katika maisha yake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post