Vera Sidika ataja idadi ya watoto anawataka

Vera Sidika ataja idadi ya watoto anawataka

Ohooo!! Mambo yamekuwa mambo bwana waswahili husema hivyo, ambapo kutoka 254 Kenya kwa  Mrembo na Mfanyabiashara Vera Sidika ameweka wazi idadi ya watoto anaotaka kuwa nao kwenye maisha yake.

Vera Sidika ameshea hilo kwenye Insta Story yake baada ya shabiki kumuuliza amepanga kupata watoto wangapi na kujibu papo hapo kuwa ni watoto watatu au wanne.

Hata hivyo ameeleza kwamba huenda mwishoni mwa mwaka huu 2022 akaongeza mtoto wa pili, kwa sasa ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Asia Brown aliyempata na mpenzi wake Brown Mauzo.

Ebwana eeeh!!! Unalionaje hilo la mrembo Sidika namna anavyopangilia kupata watoto wake? Tupe maoni yako mdau wewe unasemaje kwenye hilo/






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags