Video fupi ya MJ yafikisha watazamaji bilioni 1

Video fupi ya MJ yafikisha watazamaji bilioni 1

Video fupi ya marehemu mwanamuziki Michael Jackson (MJ) kutoka Marekani iitwayo ‘Thriller’ imefikisha watazamaji (views) bilioni 1 katika mtandao wa YouTube.

Filamu fupi ya "Thriller" sasa inaungana na video nyingine zikiwemo "Billie Jean," "Beat It," na "They Don’t Care About Us." Kufikia mafanikio hayo na kumfanya kuwa msanii wa kwanza kuwa na video nne zilizofanikiwa kufikisha watazamaji bilioni moja.

Ikumbukwe kuwa video hiyo ilitolewa mwaka 1983 na iliongozwa na John Landis, "Thriller" kwa muda mrefu imepongezwa kuwa moja ya video bora ya muziki wakati wote huku mwaka 2018 ikipewa nafasi ya kuoneshwa kwenye kumbi za sinema mbalimbali.



Video ya "Thriller" ilionesha ubunifu wa hali ya juu na hadi sasa bado inawavutia watu kutokana na video hiyo kuwa na maadhi ya Zombie huku ikiacha alama kwenye historia ya muziki.

Michael Jackson, maarufu kama "Mfalme wa Pop," aliyezaliwa Agosti 29, 1958, huko Gary, Indiana, Marekani na kufariki mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 50.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post