Wabunge kumchangia Professor Jay

Wabunge kumchangia Professor Jay

Wabunge waonesha nia ya kutaka kumsaidia aliyewahi kuwa Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye pia ni mwanamuziki wa Hip Hop, Joseph Haule maarufu #ProfessorJay.

Hii ni baada ya Professor Jay kutambulishwa bungeni Dodoma kama mgeni leo Alhamisi Novemba 09, 2023; ambapo hoja hiyo ya kumchangia ilitolewa.

Baada ya hoja hiyo kutolewa, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alitoa mwongozo kwa kila mtu kuchanga kiasi chochote alicho nacho ambapo mchango huo utakusanywa leo na kisha atakabidhiwa fedha iliyopatikana.

Professor Jay amekuwa akisumbuliwa na figo kwa takribani mwaka mmoja na miezi mitatu, hata hivyo kwa sasa afya yake inaendelea kuimarika.

Chanzo: Mwananchi

.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags