Wakali wa Hip Hop kutoka  chuo cha  Udom

Wakali wa Hip Hop kutoka chuo cha Udom

Unaambiwa siku zote bwana Nabii hakubaliki kwao  hahaha aisee huu msemo bwana unaniachagahoi sana lakini leo nakuletea Nabii ambaye ankubalika na watu wanamuelewa kinyama.

Kila chuo bwana huwa wanawakali wao kwenye Nyanja mbalimbali za sanaa kwa upande wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM wakali wao ni hawa hapaaa.

Po-Rapper na Xam Jm ni wanafunzi kutuko Chuo kikuu cha Dodoma Udom wakiwa mwaka wa pili kila mmoja wakichukua course anachukua course ya bachelor of Education in Chemistry Science.

Nikwambie tena kuwa hawa jamaa ni Manabii wanaokubalika pale mjini UDOM bwana Samson Mtowinanga pamoja na Paul Cholobi ndiyo wakali wa muziki wa hip hop chuoni hapo je wewe unakwama wapi mwamba?.

Kikubwa ukitambua kipaji chako na ukasimama nacho basi hata wa pembeni yako lazima wakuheshimu na watambue zile hustle zako katika jambo ambalo unalipigania.

Aisikwambie mtu mwananguu kama uwezo unao unao tu hilo halipingiki popote pale simama jivunie ulichonacho iaminishe jamii kisha kaapembeni utaona utakavyokubali bwana.

Po-Rapper hayuko mwenyewe kwenye hili game bhana yuko na kundi lake linalotambulika kwa jina laTHE LEGENDS ambalo ni muunganiko wa Xam Jm na Po -apper 19  likiwa chini ya usimamizi wa Ujazo Focus.  

Akiwa kama kiongozi wa kundi la The Legends Paul Cholobi anazungumzia namna walivyoanza hadi walipofikia kwa sasa.

Kwanini umeamua kuchagua kufanya muziki aina ya Rapper?

“Nimeamua kufanya Rapp coz ndiyo muziki ambao naulewa kutokana na jisi ulivyo kwenye rap unaweza kuzungumzia mambo mengi sana tena kwa wakati mmoja tofauti na bongo fleva ndiyo maana naukubali sana.”

 Je wanamuziki wa Rapper anatakiwa awe na uwezo wa kufanya Nini na Nini?

Inabidi awe na uwezo wa kufikiria kwa haraka na kutunga mashairi, awe na uwezo wakuzungumza vitu vya ukweli, ajue pia kuandika free style lakini nguzo kubwa kabisa awe anajua kuandika mashairi”

Je kipaji Chako Chimbuko lake lilikuwa wapi ?

“Mimi kipaji change bwanaa chimbuko langu nimeanzia chini kabisa tangu shule ya msingi ndipo nilipokua nikifanya vitu vyangu na kuanza kuonekana” anasema.

Umewahi kupeform kwenye show yoyote?

“Yap nimewahi kuperform kwenye show mbalimbali ikiwemo Nandi Ferstival hii iliyofanyika mwaka huu, pia kwenye matamasha yote ya NMB hapa Dodoma huwa wanatushirikisha”anasema na kuongeza.

“Hata WCB walivyokuja kupiga show hapa Dodoma tulipata nafasi ya kwenda kuperfome, pia show ya kijana mahiri nimeshashiriki namshukuru Mungu kiukweli Dodoma inanitambua vyema sana”

Vp familia inakuchukuliaje baada ya kukugundua kipaji Chako?

“kiukweli bwana kuhusu familia yangu ni watu wa dini sana hususani mama yangu mzazi hafahamu hili lakini naamini siku akigundua atanibariki tu coz napambania kipaji changu”

Je ni kitu gani ambacho hutoweza kusahau kwenye maisha Yako?

“Namna ambavyo nilikutana na watu ambao wananisupport kwenye kazi hadi sasa hivi kikubwa ni yale mazingira ambayo nilkutana no kiukweli ilikua surprise sana hilo siwezi kulisahau”anasema.

Mara nyingi wasanii wa hip hop wamekuwa wakikosoa jamiii na serikali je lazima anaeimba muziki huuu apite humo?

“Hapana nakataa kabisa sikuhizi watu wamebadilika wanaimba nyimbo za mapenzi, starehe kwa hip hop na jamii inazielewa vizuri sana hiyo ilikuwa zamani”anasema na kuongeza

“Zamani watu walikuwa wanaimba kwa kukosoa jamii na serikali zamani walikuwa wanaimba yani ni ugumu tu mwanzo mwisho lakini mabadiliko ya hip hop kwa style ya uimbaji ni mkubwa sana kwa sasa”anasema.

Jamiii inauelewa muziki wa hip hop?

“kwakweli muziki wa hip hop kwa sasa unakubalika sana hata ukiangalia kwa wasanii ambao wanaimba muziki huu akiwemo young killer, young lunya, roma mkatolic, Rostam,profesa Jay na wengine wengi hata wakitoa ngoma unaona kabisa jinsi zinavyopekelewa mitaani”anasema.

Changamoto kubwa kwenye hip hop ni ipi?

“Changamoto kubwa sana nimna utakavyoimba coz watu wameshazoea kusikiliz RNB miziki laini si unajua tena na mara nyingi hip hop wanaofatilia sana ni wanaume lakini mashabiki wa muziki ni wanawake”

“balaa liko hapo sasa kumconvience mwanamke aukubali muziki wa wa hip hop aiseee sio jambo dogo na hiyo ndiyo changamoto kubwa ninayoiyona na ndiyomaana changes zinafanyika sana kwenye huu muziki nowdays”

Owkey sawaa ukiwa kama kiongozi wa group la The legends Malengo yenu ni yapi?

Course yako unaionaje?

“Course yangu ningumu kama unavyojua mambo ya chemistry ni ngumu lakini ninapambana nayo hivyo hivyo kulingana na mambo yalivyo lakini sio sarihisi”anasema.

Vipi kuhusu changamoto ya course yako?

“Changamoto kubwa ninayoipitia sometimes unakuta mnatakiwa kwenda kuimba, au studio kurecord, kushoot video halafu kuna assignment hapo ndo napitia kipindi kigumu kidogo” anasema.

Nini kipaumbele chako muziki au elimu?

“kwakweli mimi niko tofauti sana na wengine kipaumbele change ni muziki yaani elimu nasoma lakini napenda mziki kutokana na mafanikio makubwa ninayoyana hivyo naamini nikijikita vizuri nitatoka”anasema.

Msanii Gani wa hip hop unamkubali?

“Wasanii wa hip hop ninao wakubali ni wengi lakini ninaemuelewa zaidi kuliko wasanii wote hapa bongo ni mzee mzima profesa J namkubali mnoo”anasema.

 

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags