Wakutwa hai siku 9 baada ya tetemeko la ardhi, Uturuki

Wakutwa hai siku 9 baada ya tetemeko la ardhi, Uturuki

Siku tisa baada ya maafa ya tetemeko la ardhi Uturuki na Syria, wanawake watatu na watoto wawili wamepatikana wakiwa hai.

Baadhi ya wanawake hao walitambulika kwa majina ya Melike Imamoglu mwenye umri wa miaka 42 na Cemile Kekec mwenye umri wa miaka 74 kutoka katika mji wa Kahramanmaras nchini Uturuki.

Uokoaji wao ulikuja wakati wafanyikazi walielekeza umakini wao katika kusafisha miji iliyoharibiwa na matetemeko hilo. Mamilioni ya Syria na Uturuki wanaishi katika kambi za muda na wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Video ya uokoaji iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii na Meya wa Darica, Muzaffer Biyik, ilionyesha wafanyakazi wakipiga makofi na kukumbatiana huku  Kekec akiingizwa kwenye gari la wagonjwa.

Huko Antakya mji mwingine wa Uturuki ulioathiriwa vibaya na matetemeko ya ardhi vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba mama na watoto wake wawili walitolewa wakiwa hai kwenye vifusi.

Siku kumi baada ya maafa, inakuwa vigumu kupata manusura wa tetemeko hilo na huku idadi ya vifo vilivyojumuishwa sasa imepita 41,000.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags