Wanne mbaroni kwa tuhuma za kumteka mtoto

Wanne mbaroni kwa tuhuma za kumteka mtoto

Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumteka mtoto mdogo wa kike (9) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mizengo Pinda Manispaa ya Mpanda, kisha kumfungia ndani ya chumba kwa zaidi ya siku moja wakitishia kumuua huku wakihitaji Sh50 milioni ili wamwachie.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amewataja watuhumiwa hao waliohusika na tukio hilo kuwa ni Joseph John(24), Yusuph Sadick (27) wakazi wa Mtaa wa Milupwa , Abrahamu Kassim(28) Mkazi wa Mtaa wa Misunkumilo na Samwel Nzobe (41) mkazi wa Mtaa wa Kotasi.

Amesema watuhumiwa hao wote wanne wamekamatwa kufuatia msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa ya kutekwa kwa mtoto huyo.
Kamanda Ngonyani amesema kuwa tukio hilo la kikatili limetokea June 13,2023 saa 8 kamili mchana katika Manispaa ya Mpanda wakati mtoto huyo alipokuwa anarudi shuleni kufanya usafi.

Ameeleza kuwa wakati akiwa njiani jirani na Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda watuhumiwa hao wanne walimteka mtoto huyo na kumpeleka kusikojulikana kisha kumtishia kumuua au walipwe na mzazi wake kiasi hicho cha Sh50 milioni ili wamuache akiwa hai.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags