Wanni na Handi waeleza usumbufu wanaopitia kwa wanaume

Wanni na Handi waeleza usumbufu wanaopitia kwa wanaume

Mastaa mapacha wa shoo ya uhalisia 'Reality Show Big Brother Naija’ kutoka Nigeria Wanni na Handi Danbaki wameweka wazi namna ambavyo wanaume wanawasumbua kwa kuwatongoza na kuwataka wote kwa pamoja.

Mapacha hao wamefunguka kupitia podcast ya ‘BTS’ ambapo walieleza kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni wanaume kuwataka wote kwa wakati mmoja.

“Hatujawahi kuchangia mwanaume, na hatuwezi fanya kitu kama hicho na hatuchangi mwanaume. Hili ni swala la kijinga wanaume wengi wana tamani kuwa na wanawake mapacha kimapenzi kwa wakati mmoja”

“Tulikuwa tuna tembea mtaani siku moja kuna mwanaume akasimamisha gari yake na kutuuliza kama anaweza kutoka na sisi wote kwa pamoja tulishituka”,alisema wanni

Hata hivyo kwa upande wa pacha mwingine aitwaye Handi alitilia mkazo suala hilo huku akieleza kuwa kuna baadhi ya vitu wanachangia lakini hawawezi kuchangia mwanaume.

“NDIO, wanaume wanatutaka kwa pamoja na kwa wakati mmoja. Lakini sisi hatuchangii wanaume, kuna baadhi ya vitu tuna chingia Zaidi kama nguo lakini vingine tunatofautiana kama chakula” Alisema Handi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags