Wateja waijia juu kampuni ya biscuit za Oreo

Wateja waijia juu kampuni ya biscuit za Oreo

Wateja wa muda mrefu wa biskuti aina ya Oreo wameishutumu kampuni hiyo kwa kupunguza kiasi cha cream ambayo inawekwa katikati ya biscuit hizo.

Shane Ransonet na mkewe waliishutumi kampuni hiyo kupitia mitandao ya kijamii kwa kudai kuwa siku za hivi karibuni walinunua biscuit na kukuta cream iliyopo katikati kuwa ni nyembamba sana tofauti na hapo awali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Oreo, Dirk Van de Put alidai kuwa kampuni hiyo haipunguzi kiwango cha cream kwenye biskuti ya Oreo na kudai kuwa huwenda ikawa makosa ya wafanyakazi wanaotengeneza biscuit hizo.

Mara ya mwisho kununua biscuit ya Oreo ni lini, tuambie mtazamo wako katika hili?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags