Watoto wa Murphy na Martin waunganisha undugu

Watoto wa Murphy na Martin waunganisha undugu


Wachekeshaji maarufu wa Marekani Martin Lawrence na Eddie Murphy hatimaye wamekuwa familia moja baada ya watoto wao kuchumbiana na wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

Kupitia kurasa za Instagram za watoto wa mastaa hao wamechapisha video ya kutangaza rasmi uchumba wao huku wakiweka wazi kuwa ulianza mwaka 2021.

Jasmin ni mtoto wa kwanza kati ya mabinti watatu wa Martin Lawrence na ndiye mtoto pekee ambaye mwigizaji huyo alizaa na aliyekuwa mke wake, Patricia Southall.

Kwa upande wa Eric ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 10 wa Eddie Murphy na ndiye mtoto pekee aliyezaa na mpenzi wake wa zamani, Paulette McNeely.

Ikumbukwe kuwa Martin Lawrence na Eddie Murphy ni marafiki wa muda mrefu na wamewahi kucheza katika filamu za vichekesho pamoja ikiwemo Boomerang, Life, You So Crazy na nyinginezo hata hivyo kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa wawili hao wanampango wa kutengeneza filamu ya vichekesho itakayoitwa ‘It’s a Mad, Mad, Mad, Mad World’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags