Young Thug Aomba Kurudishiwa Mali Zake

Young Thug Aomba Kurudishiwa Mali Zake

Wakati Rapa wa Atlanta, Young Thug akiendelea kupigania uhuru wake, ameiomba mahakama kumrudishia baadhi ya mali zake ikiwa ni pamoja na pesa, vito vya thamani, na magari.

Vitu hivyo vilichukuliwa na kuwekwa chini ya ulinzi baada ya rapa huyo kukamatwa Mei, 2022 kwa makosa ya utakatishaji fedha, ulanguzi wa dawa za kulevya na kuendesha Genge la wahuni.

Rapa huyo kutokea Georgia, Atlanta inaripoti kwamba alipangiwa kusikilizwa Ijumaa Februari 21, 2025 kuhusu suala la kurudishiwa vitu vyake. hata hivyo usikilizwaji wa madai hayo ulisitishwa.

Miongoni mwa vitu ambavyo Thug na mawakili wake wanajaribu kurejeshewa ni Pamoja na pesa taslimu Dola 149,426 , vito vya thamani na magari kadhaa ambayo kulingana na rekodi za mahakama, ni pamoja na Dodge Durango ya 2021, Porsche 911 ya 2022, Mercedes-Benz GLS Maybach ya 2021, Can-Am Spyder ya 2015 na Chevrolet Corvette ya 2022.

Utakumbuka rapa Young Thug aliachiwa na kupewa kifungo cha nje Novemba 1, 2024 akinusulika kutumikia kifungo cha miaka 40 jela baada ya kukiri makosa yake. Hata hivyo alipewa masharti ya kufuata ikiwa ni pamoja kutojihusisha na magenge ya wahuni, kufungwa kifaa mguuni kitachotoa taarifa ya mwenendo wake .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags