Zaidi ya watu 200 wauwawa kwenye mapigano ya kikabila, Sudan

Zaidi ya watu 200 wauwawa kwenye mapigano ya kikabila, Sudan

Afisa mmoja wa juu wa afya nchini Sudan Fath Arrahman Bakheit amesema mapigano ya siku mbili ya kikabila kusini mwa nchi hiyo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 220.

Mapigano hayo yaliyozuka katika mkoa wa Blue Nile, unaopakana na Ethiopia na Sudan Kusini, yalizuka tena mapema mwezi huu kuhusiana na mzozo wa ardhi, kati ya kabila la Hausa lenye mizizi yake Afrika Magharibi, na watu wa kabila la Berta.

Kulingana na Fath Arrahman Bakheit, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa wizara ya afya katika mkoa wa Blue Nile, mzozo huo ulipamba moto siku ya Jumatano na Alhamisi katika mji wa Wad el-Mahi, ulioko kwenye mpaka na Ethiopa.

Bakheit amesema maafisa walihesabu maiti zisizopungua 220 kufikia Jumamosi usiku, na kuongeza kuwa huenda idadi inaweza kuwa kubwa zaidi, kwa sababu timu za madaktari hazikuweza kufika kwenye kitovu cha mapigano. Maafisa zaidi wa usalama wametumwa eneo hilo la Wad el-Mahi na vilevile amri ya kutotembea nje usiku imetangazwa eneo hilo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags