Siku nyingine tena kwenye dondoo za mitindo na urembo. Leo tunaangalia mambo yakuzingatia wakati wa ubandikaji kucha.
Ubunifu kwenye masuala ya urembo wa kucha umezidi kukua, ikiwa kama njia mbadala kwa watu wasioweza kufuga kucha.
Ubandikaji wa kucha umekuwa ukifanyika kwa aina tofauti tofauti, cha muhimu unachopaswa kuzingatia ni unapenda kucha zako ziwe katika muonekano gani, pia unapaswa kutambua rangi itakayoweza kuendana na ngozi yako ya kucha ili uvutie zaidi.
Unashauriwa kujua ni aina gani ya gundi itakayotumika kuwekwa katika kucha ili usipate madhara, pia wakati wa kutoa hakikisha unaweka mikono yako yenye kucha bandia katika maji ya uvuguvugu na kubandua taratibu ili usipate madhara.
Aidha inaelezwa kuwa zipo dawa ambayo hutumika kubandulia kucha iliyobandikwa pindi utakapokwenda kwa mbandikaji lazima atakuwa nayo.
Licha ya urembo huu kupendwa na watu wengi lakini wataalamu wa afya wanasema umekuwa ukisababisha athari kwa watumiaje wake endapo urembo huo utabandikwa kwa gundi zisizofaa.
Madhara yanayoweza kusababishwa na ubandikaji kucha.
*uvimbe
Kuna baadhi ya kemikali zinazotumika kubandikia au kuondoa kucha bandia zinaweza kusababisha miwasho kwenye ngozi yako na kuwa nyekundu hali ambayo inaenda kusababisha uvimbe kwenye kucha na kupata ugonjwa wa ‘resini’ ambao umehusishwa na saratani.
Nini unaweza kufanya ili kuzuia madhara hayo?
*ikiwa unapenda kubandika kucha bandia jaribu kusitisha ubandikaji huvyo kwa muda wa miezi kadhaa, yaani ipe muda wa kuwa huru kucha asili.
*Chagua saluni ambayo unaamini inaweza kubandika kucha vizuri na kuzingatia upakaji wa rangi ya jeli kwa taa za ‘leed’ ambazo haziathiri kucha natural, usiwe na utaratibu wa kubadilisha salooni kila wakati.
*Usikae na kucha bandia kwa zaidi ya week mbili ili kuepuka uharibifu wa kucha pamoja na ngozi yako .
*Unashauriwa kuweka kucha bandia katika matukio muhimu ili kuepuka uharibifu wa kucha zako kama sherehe za harusi, party au event mbalimbali zitazohusisha kuwa mrembo na mwenye muonekano mzuri.
Nb. Usiweke kucha bandia juu ya kucha yako natural ikiwa ndefu inayolingana na kucha bandia.
Leave a Reply