Wakati wimbo wa mwanamuziki Zuchu aliomshirikisha Diamond ‘Wale Wale’ ukiendelea kufanya vizuri kwenye mitandao ya kusikiliza muziki huku ukishika nafasi ya tatu kwenye mtandao wa YouTube, Zuchu amechukua mistari kwenye moja ya nyimbo za marehemu kaka yake Omary Kopa.
Zuchu kupitia wimbo wake huo uliotazamwa zaidi ya mara laki tano, ametupia mstari ambao umewahi kusikika kwenye wimbo wa marehemu kaka yake uitwao ‘Imetulia Hiyo’ huku akichukua mstari usemao “Chote ni choyo usijali wao kitawaumiza”, mbali na kuchukua mistari hiyo pia melodi za nyimbo hizo mbili zinaendana.
Aidha Zuchu si tu kuchukua mistari kwenye baadhi ya ngoma za marehemu kaka yake pia huenda akawa anatumia majina ya nyimbo za Omary ikiwemo ‘Hakuna Kulala’ ambalo ni jina la wimbo aliowahi kutoa Omary miaka ya nyuma.
Omary Kopa alifariki dunia March 26, 2007 akiwa na umri wa miaka, alizikwa siku inayofuata Visiwani Zanzibar, aliwahi kutamba na nyimbo kama Ee Bwana Ndiyo, Kindumbwe Ndumbwe, Nifagilieni, Mambo Hadharani, Kama Noma na nyinginezo.
Leave a Reply