50 Cent aingilia kati bifu la Drake, Kendrick Lamar

50 Cent aingilia kati bifu la Drake, Kendrick Lamar

Baada ya ‘rapa’ Kendrick Lamar kutoa ngoma kwa mpigo kwa ajili ya Drake, mwanamuziki huyo naye amejibu mashabulizi hayo kwa kutoa ngoma mpya siku ya jana iitwayo ‘Family Matters’ ambapo kufuatia na bifu hilo, ‘rapa’ 50 Cent ameingilia tena kati kwa kudai kuwa aliwaambia baadhi ya mastaa wamuache Drake lakini hawakusikia.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa 50 ame-share kipande cha ngoma ya Drake akieleza kuwa ‘Nliliwaambia muacheni huyu jamaa ona sasa kila mmoja ni lazima afe”

Hii siyo mara ya kwanza kwa 50 kuingilia kati mabifu ya watu, wiki kadhaa zilizopita aliingilia bifu la Quavo na Chris Brown ambapo alidai kuwa mabifu hayo yapo katika hatua mbaya na yanauwezekano mkubwa wa kuharibu biashara ya muziki nchini Marekani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags