Wakati Rais wa Marekani, Donald Trump akionesha nia ya kutaka kumsaidia rapa Diddy dhidi ya mashitaka yanayomkabili. 50 Cent anaonesha kupinga kwa kukumbushia baadhi ya matukio yanayomuonesha Diddy akimdhiki Rais huyo.
50 Cent anatumia kauli za Diddy za kibaguzi dhidi ya Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump ili kutibua mpango wa Trump wa kumpa msamaha wa Rais na kumtoa jela Diddy, ikiwa ni pamoja na ile aliyosema "Watu weupe kama Trump wanatakiwa kufukuzwa"
Trump ameonesha nia ya kumsaidia Diddy siku za hivi karibuni ambapo rapa 50 Cent amepinga vikali na akaahidi kutoa video za Diddy akimuongelea vibaya Trump tena akishinikiza Rais Trump kufukuzwa.
50 Cent ambaye amekua na ushawishi mkubwa sasa amechukua hatua hio kama sehemu ya kumuonesha Trump kwamba mtu anayetaka kumtoa jela alikuwa na uadui mkubwa dhidi yake wakati yupo uraiani.
Hata hivyo Desemba 7, 2023, 50 Cent alitangaza kuwa ameandaa makala maalumu ya 'Diddy Do It' inayoelezea maovu yaliyofanywa na Diddy ambapo inatarajiwa kuoneshwa kupitia NetFlix. Makala hiyo ilitangazwa tena wiki moja baada ya Diddy kukamatwa Septemba 2024 na itaangozwa na Alex Stapleton.
Sababu kubwa ya ugomvi kati ya 50 Cent na Diddy inatokana na diss track aliyoachia 50 Cent mwaka 2006, iitwayo 'The Bomb'. Katika wimbo huo, 50 Cent alisisitiza kuwa Diddy anajua kitu kuhusu mauaji ya rapa The Notorious B.I.G. pamoja na matukio mengine

Leave a Reply