“Habari ndugu zangu Watanzania Leo ningependa kuongelea hili swala la Watu kunihusisha na uchochezi wa vitu vibaya Kati yangu mimi na Paten, mimi huyu ni mwanangu familia yangu na sipendi watu wanavyozidi kunihusisha mimi na mambo ya kishirikina.
Nimeona clip ikisambaa kuwa kashindwa kuimba huenda ni wingi wa kazi ndio maana inatokea hivyo sisi sote ni watoto wa kimskini tunatafuta riziki, Mungu kaamua kumfungulia kwa upande wake na mimi Mungu anabariki napata riziki na sina ugomvi nae huyo ni ndugu yangu na wale mlionihusisha kuwa nimemkausha sauti hivi vitu sivipendi na vinaniumiza sana ningependa tu niwaombe ndugu zangu tusapotini mziki mzuritusapotini wote Asante,”ameandika Paten

Utakumbuka siku moja iliyopita kulisambaa video za Paten kushindwa kutumbuiza baada ya kupata changamoto ya suati kukauga ghafra wakati alipokuwa kwenye mkesha wa Mwenge uliyofanyika Gongo La Mboto.
Kutokana na hilo kumekuwa na komenti nyingi katika video hiyo baadhi ya mashabiki wakimuhusisha Sajent kuhusika na tatizo hilo “Sajent huyo tumkabe atatueleza kwanini yeye sauti bado anayo”, “Uyo ni Sajent mizimu ya nyumbani imeniambia,” “Mazombi ya Sajent hayo lakini hatuumi tupo na lasta born wa Taifa”, huku wengine wakiandika “Sajent akibanwa atasema kwanini amefanya hivi,”.
Aidha kwa upande wa Paten kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshare ujumbe kuhusiana na tatizo la kushindwa kutumbuiza akiandika “Asanteni sana mashabiki zangu wa Gongo La Mboto, mniwie radhi kwa changamoto ya sauti usiku wa jana. Tusisahau kuumwa ni Ibada na kila alieumbwa lazima ajaribiwe na Mola wake,”ameandika
Leave a Reply