Wimbo pendwa wa Singeli kutoka kwa mashabiki hasa watumiaji wa mtandao wa TikTok ‘Afande’ ulioimbwa Dogo Paten akimshirikisha Zuchu umetajwa kuwania tuzo za ‘EAEA Awards’.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Paten ameshare taarifa hiyo akiandika “Siamini! Ngoma yetu pendwa imeteuliwa kwa mara ya kwanza kwenye tuzo za @eaea_awards_inc as Best Singeli Fusion kupitia wimbo wangu Afande niliomshirikisha dada @officialzuchu .
Hii ni neema, ni baraka, ni motisha kubwa sana kwangu. Mchakato wa kupiga kura bado haujafunguliwa, lakini naombeni naomba sana usaidizi wenu muda ukiwa tayari. Nahitaji hii tuzo kama kumbukumbu yangu,”ameandika Paten
Ukiwa na siku 12 tangu kuachiwa kwakwe katika majukwaa ya kuuza na kusikiliza muziki wimbo huo unaendelea kupata mafanikio makubwa huku ukikubalika zaidi ndani na nje ya nchi.
Mbali na wimbo huo kumtambulisha rasmi Paten kwa Watanzania lakini pia msanii huyo amekuwa akiwavuruga mastaa na wadau mbalimbali wa burudani huku jina lake likitajwa Bungeni kutokana na vibe alilolionesha kwenye ‘Samia Serengeti Music Festival’.

Leave a Reply