Albumu ya Kanye na Dolla yaondolewa Apple music

Albumu ya Kanye na Dolla yaondolewa Apple music

Albamu ya ‘rapa’ Kanye West na Ty Dolla $ign ‘Vultures 1’ inadaiwa kuondolewa kwenye mtandao wa kuskiliza muziki wa Apple Music na iTunes siku tano baada ya kuachiwa kwa mara ya kwanza.

Album hiyo imeondolewa kwenye mitandao hiyo kutokana na kuiba sampuli (copyright) za nyimbo za wasanii wengine akiwemo Donna Summer na Keyshia Cole ambao walidai kuwa kazi zao zilitumiwa bila idhini yao.

Ikumbukwe kuwa ‘Vultures 1’ Albumu yenye nyimbo 18 iliachiwa rasmi Februari 10, mwaka huu katika platform zote, huku wimbo wa ‘Carnival’ ukiwa unashika namba moja kwenye chati 100 bora.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags