Aliyejaribu challenge ya kuzikwa akiwa hai, atoka mzima

Aliyejaribu challenge ya kuzikwa akiwa hai, atoka mzima

Kijana mmoja kutoka nchini Nigeria aliyetambulika kwa jina la Young C, ametoka akiwa mzima baada ya kuzikwa kwa saa 24.

Kijana huyo alitangaza kufanya tukio hilo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram siku ya Jumatano Mey 8, mwaka huu na kufukuliwa siku ya jana Alhamisi Mei 9, akiwa hai.

Wakati akiwa ndani ya sanduku hilo aliwasiliana na rafiki zake kwa njia ya meseji ili kujua kama yuko salama pamoja na ku-share ujumbe katika Instagram yake kwa ajili ya kuwajuza mashabiki zake kuwa yupo hai licha ya kupata usumbufu wa kimwili na kukosa maji.

Young C amefuata nyayo za mtengenezaji maudhui kutoka Marekani aitwaye Jimmy Donaldson maarufu Mr Beast aliyevunja rekodi ya kuzikwa na kutoka akiwa hai ndani ya siku saba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags