‘Bodi’ ya ‘Ligi’ Tanzania Bara imemtangaza #AhmedArajiga kuwa mwamuzi wa mchezo wa Kariakoo Dabi ambao ni #Simba na #Yanga utakaochezwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mchezo huo utawakutanisha wababe hao wawili wa #Kariakoo ambapo #Simba ndiye mwenyeji huku ‘mechi’ hiyo ikitarajiwa kuanza Saa 11:00 jioni.
#Simba itaikaribisha #Yanga ikiwa ni dabi yao ya pili msimu huu wa 'ligi' baada ya ile ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Agosti jijini Tanga, #Simba ikibeba ngao hiyo.

Leave a Reply