Aziz KI athibitisha ndoa yake na Hamisa

Aziz KI athibitisha ndoa yake na Hamisa

Dakika chache baada ya kiungo wa Yanga, Stephanie Aziz KI kutupia kambani chuma tatu, furaha yake imemfanya kufichua juu ya ndoa yake na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Azizi Ki amefunga mabao matatu yaani hat trick kwenye ushindi wa mabao 6-1 ilioupata Yanga dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mara baada ya ushindi huo, Aziz KI akizungumza na Yanga Tv amethibitisha kwamba furaha yake kubwa ya kiwango alichoonyesha inakwenda sambamba na tukio la ndoa yake itakayofanyika kesho, Februari 15.

"Ni siku nzuri kwangu leo kwa sababu kesho nitafunga ndoa. Kwa hiyo naitoa tuzo hii kwa mke wangu Hamisa, bebi hii ni kwa ajili yako," amesema Azizi Ki huku akionyesha tuzo ya mchezaji bora wa mchezo aliyoitwaa baada ya mechi hiyo.

Hata hivyo, mchezaji huyo hakufafanua zaidi juu ya ndoa hiyo ambayo imekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.

Wakati Azizi KI akithibitisha hilo, Mobeto mwenyewe anafanya yake kwenye ukurasa wa Ista story katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Mrembo huyo mara baada ya mchezo huo ameweka picha ya Aziz KI akiinama kumshukuru Mungu, huku akibandika maneno machache 'aah jamani mume wangu'.

Mapema kulienea uvumi kwamba Aziz KI atafunga ndoa na mwanamitindo huyo huku baadhi ya mabango yakiwekwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam kwamba wawili hao watafunga ndoa Februari 15 au 16.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags