Mwanamuziki wa Bongo Fleva, B2k Mnyama ameweka wazi changamoto alizopitia mpaka kusimama na kutambulika kwenye ramani ya muziki wa Bongo Fleva.
Akizungumza na Mwananchi Scoop, B2k amesema alimchukua muda kutambulika na kupewa sapoti kwa sababu wadau wengi hawakumpa heshima anayostahili kisa ni msanii aliyetokea mkoani.
"Changamoto huwa zinakuwa nyingi sana husasani ukishatokea unatokea mokoani yaani hawawezi kukupa heshima unayotakiwa kupewa. Mimi nimetumia nguvu kubwa kupata hii heshima ambayo napewa, hata watangazaji ambao wanatokea kusini wakifika mjini wakapata nafasi fulani wanakuchukulia wa mkoani hawawezi kukupa sapoti kama wewe ni wa nyumbani," amesema B2k.
Amesema alitumia zaidi ya miaka sita mpaka kutengeneza jina lake akiwa ukanda wa kusini mwa Tanzania, mkoani Njombe sehemu alipoanzia sanaa yake.
"Zaidi ya miaka sita nimepambana kutengeneza jina langu. Kwanza nilianzia Makambako nikaja mkoa wa Njombe na Kusini kiujumla na baadaye nikafahamika Tanzania nzima ila ilinichukua zaidi ya miaka sita mpaka kujitengeza mwenyewe na kutambulika nje ya ukanda wa kusini nilipoanzia," amesema B2k.
Amesema changamoto hiyo ya kutopata nafasi ilipelekea kuingia kwenye shoo za Chaka tu Chaka ambazo zimemsaidia kuinuka kimaisha kabla ya kuanza kufanya shoo kubwa mwaka 2024.
"Chaka tu Chaka zimeongeza hadhi yangu kwa sababu kwanza nakutana na mashabiki ambao naimba nao moja kwa moja. Pia nimejenga Dar kwa sababu ya Chaka tu Chaka
nyingi wasanii kuliko shoo za matamasha makubwa.
"Unajua kwenye maisha ya Chaka tu Chaka ukifika popote pale utakutana na vitu vingi sana. Unaweza kwenda mkoa fulani mtu kakulipa pesa alafu ukifika tuu unaweza kupata shoo wiki nzima kwa sababu vijijini watu hawasubiri Weekend," amesema.
B2k anasema Chaka tu Chaka zipo mpaka za Kimataifa kwani Julai 2025, alienda kupafomu Uganda, Rwanda na Burundi.
"Kwanza nilipata shoo Karagwe nikapata shoo Uganda pale mpakani, nikapata na Rwanda. Lakini nitaenda tena Septemba 6, 2025. Wanazijua tu nyimbo lakini msanii hawamjui, kwa hiyo mkiwa kwenye matangazo mtaani wimbo ukipigwa ndio wanajua kumbe ameimba huyu unajua zile ni nchi za watu wanasikiliza sana nyimbo kuliko kumfuatilia msanii," amesema B2k.
Amemaliza kwa kusema kazi yake iliyogharimu kiasi kikubwa cha pesa ni Lala aliyomshirikisha Vanillah.
"Ni collabo na Vanillah ile ya kwanza inaitwa Lala ni moja kati ya projekti ambayo nilitumia gharama sana. Kwanza tulitoa video mbili ambazo tulishuti kwa watu tofauti tofauti, vyote hivyo nilitumia hela nyingi kupush ile kazi na ninashukuru Mungu iliondoka pia," amesema B2k.

Leave a Reply