Bei ya mahindi yapanda zaidi

Bei ya mahindi yapanda zaidi

Ripoti ya mapitio ya uchumi ya August, 2022 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema bei ya gunia la mahindi la Kilo 100 kwa mwaka ulioishia July 2022 ilikuwa Tsh. 87,383 ikipanda kutoka Tsh. 43,371 iliyorekodiwa kipindi kama hicho mwaka 2021.

Aidha kuna ongezeko kwenye mazao mengine ndani ya kipindi hicho kwa gunia moja ambapo mchele ni Tsh. 67,365 na maharage Tsh. 21,047 na mtama ni Tsh. 26,184.

Ripoti imeonesha hali hiyo imechangiwa na kuongezeka kwa mahitaji ya mazao hayo hasa nje ya nchi na kutokuwepo kwa mvua za kutosha nchini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags